Waziri Mkuu Atua Dodoma Kwa Ndege ya Abiria

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria vikao vya bunge  ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho Jumanne

Waziri Mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayopitia Dodoma kuelekea Kigoma

Katika Uwanja wa Ndege Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wa serikali na chama wa mkoa wa Dodoma

Vikao vya Bunge vinaanza kesho baada ya wiki mbili za shughuli za kamati za kudumu za Bunge, na sasa tayari wabunge wamekwishawasili Dodoma kwa ajili ya vikao hivyo vitakavyodumu kwa takriban wiki 2


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo