Wakazi wa kijiji cha Kipanga Wilayani Kalambo Rukwa wamemvamia mwalimu wa shule ya Msingi Kipanga Musa Mbosa na kumpiga na fimbo, marungu wakimtuhumu kuwabebesha vipande vya tofali watoto wao
Mkuu wa shule hiyo Enock Majenga alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya mwalimu huyo kuwapa adhabu wanafunzi ambao hawakuhudhulia kazi ya kusogeza tofali kwenye choo cha shule ambacho kilikuwa kinaendelea kujengwa
Alisema wakati wa likizo aliwaahidi wanafunzi hao kwenda shule kwa ajili ya kusomba tofali hizo, lakini kuna wanafunzi wengine hawakufika
“Shule ilipofunguliwa mwalimu Mbosa alaimua kuwaadhibu wanafunzi ambao walishindwa kufika kwenye kazi hiyo lakini baada ya muda mfupi baadae kundi la wananchi wakiwemo wazazi wa wanafunzi walifika shuleni na kumvamia mwalimu huyo na kuanza kumpiga na kumsababishia maumivu makali sana.”