
Wakazi wa mtaa wa Mivinjeni Buguruni jijini Dsm wakiongozwa na baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa huo wamepeleka malalamiko yao kwa maandishi kwa Afisa mtendaji wa kata hiyo ya kutokuwa na imani nae m/kiti wao wa mtaa huo baluwa mwakilanga kwa tuhuma mbali mbali zikiwemo za miradi katika mtaa wao.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mtendaji kata eneo la buguruni chama wananchi hao wamedai m/kiti wao amekuwa Mbabe katika utendaji kazi,lakini pia amewatimua wajumbe watatu wa mtaa huku pia wakitilia mashaka miradi ya visima Tisa ambavyo wamedai ni kimoja tu kichochimbwa katika mtaa wao.
Afisa Mtendaji wa kata ya Buguruni Remi mwinshehe ambaye amepokea malalamiko hayo ambayo pia wananchi 400 wametia saini kumlalamikia amesema watafanyia Uchunguzi wa kina tuhuma hizo ,huku m/kiti anayelalamikiwa akizungumza na Chanel ten amepinga tuhuma zilizotolewa dhidi yake na kudai kuwa ni njama za wabaya wake kisiasa wanataka kumchafua.