Anna Senkoro afariki dunia, Aliwahi kugombea Urais mwaka 2005


Aliyekuwa mgombea urais wa kike wa kwanza Tanzania kwenye Uchaguzi mkuu wa 2005 kupitia chama cha APPT-Maendeleo, Dr. Anna Claudia Senkoro amefariki dunia nyumbani kwake Tabata Segerea jijini Dar es salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Marehemu Anna aliugua ghafla jana usiku na kukimbizwa hospitali kabla ya mauti kumkuta. Mwili wa Marehemu Umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili kusubiri taratibu za mazishi.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo