Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo Nchini kupitia Gazeti la UHURU, Amina Athuman amefariki Dunia Asubuhi ya leo huko Visiwani Zanzibar wakati akipokea matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Awali, taarifa zilizopatikana kupitia kwa watu wa karibu wanahabari wenzake waliopo huko Zanzibar waliomba maombi zaidi kwa wanatasnia ya habari ambapo alikuwa amelazwa hospitalini hapo.
“Jamani wanagroup tumuombeeni dua mwenzetu amina athumani hali yake sio nzuri huko zanzibar na sasa hivi kalazwa hospital ya mnazi mmoja (Ujumbe wa usiku )
“Leo asubuhi alipatwa na maumivu makali tumboni ambapo alidai yanapanda hadi kifuani ikabidi akachomwe sindano yakutuliza maumivu lakini haikusaidia zaidi alipata maumivu zaidi na kuagaragara huku akitoka damu mdomoni.
Kwa mujibu taarifa za awali alionekana kupata dalili za kifafa cha mimba lakani kwa taarifa zilizopo kwa sasa anaasilimia kubwa ya kufanyiwa operesheni ili kuokoa maisha yake na ya mtoto, tumuombee dua Inshaallah kwa uwezo wa Allah amvushe katika hali hii (taarifa ya alfajili ya leo)
Hata hivyo katika kuokoa uhai wake na mwanae, madaktari walifanikiwa kumtoa mtoto ambaye alikuwa wa kiume na baadae taarifa za kufariki kwa mama (Amina).
Marehemu amepatwa na umati huo wakati akiwa visiwani Zanzibar kuripoti michuano ya Mapinduzi Cup 2017 yaliyomalizika usiku wa 13 Januari.
Marehemu pia kabla ya kufanyia kazi gazeti la Uhuru, awali alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Business Times kupitia magazeti ya Majira.
Taarifa za hivi punde: Mipango ya mazishi ipo Kariakoo mkabala na kanisa la Walokole. Tafadhali wanahabari na wadau wa michezo wanajulishwa ikibidi tujumuike na jamaa wa marehemu katika tukio hili zito. Ahsante. (Mwinyimvua Nzukwi – Mwenyekiti ZASWA).
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa…
Bwana alitoa na Bwana ametwaa JIna lake Lihimidiwe.
AMEEN