Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Mkuu wa Magereza kamishna Juma Malewa wakizungumza na Waandishi wa Habari leo katika gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam.
.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege katika gereza hilo la Ukonga,jijini Dar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa,mara baada ya kukagua Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.
Na Anthony John Glob Jamii.
NAIBU Waziri mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la zimamoto na Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake wakashone katika jeshi la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.
Masauni ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kutembelea Magereza Ukonga,jijini Dar, ambapo amekagua Kiwanda cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.
Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito kwa Watanzania kwa kununua bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Aidha amewapongeza askari wa jeshi la Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Naye kaimu Mkuu wa Magereza Kamishina Msaidizi . Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama mashine za kushonea nguo, na mashine za za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo, hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.