NA KENNETH NGELESI,MBEYA
KATIBU Mkuu wa chama Kipya cha kutetea haki na maslai walimu Tanzania (CHAKAMWATA), Meshack Kipange wamekusudia kuziburuza mahakamani Halmashauri nne za mikoa kadhaa nchini, kwa madai ya kukataa kutii sheria ya ajira na mahusiano kazini , ambapo zimeendelea kukata makato ya asilimia mbili kwa walimu 617 waliojitoa CWT na kujiunga na hicho kipya.
Akizungumza nasi jijini hapa Kapenge alisema kuwa Kusudio hilo lilifikiwa juzi kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho, ulioandaliwa kwa pamoja na viongozi wa mikoa ya Mbeya na Songwe na kufanyika katika Hoteli ya Mfikemo , Jijini Hapa, na kwamba tayari chama hicho kimeshatoa notisi ya kuzifikisha mahakamani Halmashauri hizo.
Alisema kuwaMchakato umeshafanyika baada ya kuandika barua mbili zenye kumbukumbu namba CMC/TU.031/ED/08 ya Septemba 5 mwaka 2016 kwenda kwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais, pamoja na barua CMC/TU.031/ED/03 kwenda Tamisemi wakilalamika juu ya Wakurugenzi kukaidi agizo la kisheria.
Alisema mbali na kuvunja sheria, pia Wakurugenzi hao wamekaidi agizo la Rais Dk. John Magufuli alilolitoa mwaka jana katika kilele cha sherehe za wafanyakazi nchini (Mei mosi) la kutaka walimu na wafanyakazi wengine wasilazimishwe kujiunga na vyama vya wafanyakazi ambavyo si chaguo lao.
Kapange alizitaja Halmashauri hizo ambazo zimeendelea kukata makato ya asilimia mbili yanayowasilishwa CWT badala ya CHAKAMWATA ni Halmashauri ya Mbeya Vijijini ambao jumla ya walimu ni 365.
Nyingine ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya walimu 135, Manispaa ya Iringa walimu 68, pamoja na Halmashauri ya Kigoma Ujiji walimu 47 ambao kwa takribani mwaka mmoja sasa makato yao yamekuwa yakikatwa na kwenda CWT badala ya CHAKAMWATA.
“Halmashauri inapaswa kutii tamko la kisheria la kukata asilimia moja tu ya walimu hao waliojitoa CWT na makato haya kuwasilishwa CHAKAMWATA kwani kimeanzishwa kisheria na walimu hao walijitoa na kujiunga kwenye chama kipya kwa hiari yao.”.
Alisema Tanzania kwa sasa inavyama vitatu vya walimu ambavyo alidai ni vichache ukilingfanisha na baadhi ya nchi kama Nigeria yenye vyama vya walimu 47, Kenya vyama vitatu, Uganda vyama nane na Burundi vyama vitano.
Katika hatua nyingine Makamu mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Iddi Ndudi, ameitaka serikali kulipa madeni yote ya walimu kwa kuwa tayari imemaliza zoezi la kuhakiki watumishi hewa.
Naye Katibu wa chama hicho, Mkoa wa Mbeya na Songwe, Edger Chahe , alitaka viongozi wa serikali kuingilia kati na kuwachukulia hatua baadhi ya wakurugenzi watendaji wanaojipambanua wazi kukipinga chama hicho kwa maslahi binafsi.