
mtoto huyo (19) akiwa amekaa kwenye mkeka akiongea na waandishi wa habari


Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akimpa pole mtoto huyo


Nyumba alipokuwa anaishi Sikujua Pesambili

Tuma Kitaba Msamaria mwema anaemtunza kwa sasa binti huyo

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akiongea na wanakijiji cha kiwanja kata ya mbugani wilayani Chunya

Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Chunya

MWANAUME mmoja alijulikana kwa jina
la Maneno Pesambili Kanjanja (anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani
Chunya akituhumiwa kumfanya binti yake wa kumzaa kuwa mke ili hali ni mlemavu
wa miguu kumnyanyasa.
Mwanaume huyo ambaye haelewani na
majirani kutokana na ukali na alikamatawa Januari, 22 mwaka huu majira ya
saa mbili usiku kitongoji cha mwakambonja kijiji cha kiwanja kata ya
mbugani hapa.
Kwa mujibu wa majirani wa Mtuhumiwa
huyo walisema walimuona binti huyo (19)akiwa anatambaa ya saa moja
akitokea katika nyumba yao na kuelelea katika ghofu nyumba iliyopo mita
100.
Walisema walipomuuliza alikokuwa
akielelea ndipo alipowajibu alikuwa akienda kujihifadhi kwa hakutaka
kurudi tena kwenye nyumba baba yake kwa madai kuwa alikuwa akimnyanyasa na
kumtesa pamoja kumuingilia kimwili bila kumpatia huduma yoyote.
Walisema kutokana na hali hiyo
waliingiwa na huruma na kuamua kuripoti katika ofisi ya Kijiji ambapo kwa
pamoja walimsaka mwanaume huyo na kufanikiwa kumpata na kisha kumfikisha
katika vyombo vya dola huku taratibu za kumfanyia usafi binti zikiendelea
kutokana na hali yake kudhoofu na kunuka mwili wake.
Akisimulia mkasa huo mbele ya
waandishi wa habari binti huyo [19] alisema vitendo vya kikatili vilianza
baada ya mama yake kufariki akiwa mdogo ambapo alilazimika kukatiza
masomo akiwa darasa la sita shule ya msingi kiwanja kutokana na
kukosa chakula na mahitaji ya shule kama sare na madaftari.
Alisema hali hiyo
ilipelekea yeye kufanya vibarua kama kulima, kuuza bar na kuchimba dhahabu
ili kujikimu kwa chakula yeye na wadogo zake wanne waliokuwa hawapati
mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Aidha alisema baada ya kuchoshwa na
vitendo hivyo binti huyo aliacha masomo na kuolewa Jijini Mbeya akiwa na
miaka kumi na nne ambapo waliishi na mumewe kwa miaka mitatu ndipo
Mumewe alipokamatwa kwa wizi kasha kufungwa ndipo yeye
aliamua kurudi nyumbani kwa baba yake wakati huo akiishi Chalangwa
akifahamika kwa jina la Maneno Pesambili Kanjanja.
“Baadae tulihamia kijiji cha Kiwanja
huku baba akiendelea kunitesa na kukumbwa na ulemavu wa miguu na baba
akawa ananifungia ndani na kuniingilia kimwili mbele ya wadogo zangu
watatu kwa zaidi ya miezi miwili sasa licha ya ulemavu wa miguu”
alilalamika binti huyo.
Aliongeza kuwa amekuwa akifanya
ukatili pia amekuwa akimnyima chakula na maji pia alianza kumnyanyasa
baada ya kuona ananuka sehemu za siri kutokana na kukosa maji ya
kujisafisha wakati wa hedhi na kuanza kumtukana kuwa ni jinni linanuka.
Kutokana na ukatili huo wanachi hao
walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Gideon Kinyamagoha ambaye
alimhoji Mtuhumiwa lakini hakuridhishwa na majibu ndipo alioamua kuwasilana na
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Chunya Theresia Mwendapole kwa hatua za
kisheria.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii
amekiri kupokea suala hilo na kutoa taarifa Polisi ambapo walifungua
jalada la uchunguzi kwamba mwanaume huyo ameshindwa kuhudumia familia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Chunya, Rehema Madusa alithibitisha kuweo kwa tukio hilo licha ya kukiri
kuwa alipata taarifa kupitia kwa waandishi wa habari waliofika kufuatilia tukio
hilo la unyanyasaji.
Hata hivyo Madusa alilazimika
kufuatilia kwa kina jambo hilo na alipofika Kijijini hapo ambapo
alikutana na Serikali ya Kijiji na Kata, Kaimu Mtendaji Kata Tegemea Kaminyoge
alisema alimfahamu mtuhumiwa akiwa Chalangwa kabla ya kuhamia hapo.
Akiongea na Mkuu wa Wilaya binti huo
alikiri kufanyiwa vitendo vya kikatili na baba yake kwa kunyimwa chakula
na kuingiliwa kimwili.
Mkuu wa Wilaya, Madusa baada ya
kujiridhisha na hali halisi ameliagiza Jeshi la polisi kubadilisha
mashitaka ya kumwingilia kimwili badala la lile la awali la kushidwa kutoa
matunzo kwa familia.
Aidha Madusa alimwagiza Afisa
ustawi wa jamii kumpeleka hospitali binti huyo na kupimwa vipimo vyote
pamoja na mtuhumiwa ikiwa ni sambamba watoto wengine watatu wa Maneno Pesambili
wanaoishi hapo akiwemo wa kiume mwenye umri wa miaka sita aliyekatisha masomo
na kuajiriwa kuchunga ng’ombe ili kubaini kama kuna magonjwa wameambukizwa.
Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa
Serikali itahakikisha inasimamia kwa hali na mali matibabu ya binti huyo
ili aweze kutibibiwa na kurejea katika hali yake ya awali.
“Nitoe wito kwa jamii tuendelee
kushirikiana katika kundoa maovu katika jamii zetu kwa kuwafichua mapema
wahusika kabla hawajaleta madhara, huyo tutamtibu na atapona hayo macho ni kwa
ajili ya kufungiwa ndani kwenye giza pia mhusika kule ameshafika msiwe na
wasiwasi” alisema Madusa.
Chanzo: Mbeya yetu