Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Singida ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe, ameongoza viongozi mbalimbali wa serekali, wadini, polisi, magereza, jeshi la wananchi pamoja na wakazi wa Singida katika kuaga mwili wa kamanda wa polisi mkoa wa Singida marehemu SACP Peter Kakamba aliyefariki tarehe 29 Novemba katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar-es-Salaam.
Akiongea kwaniamba ya mkuu wa mkoa wa Singida katibu tawala wa mkoa wa Singida daktari Angelina Lutambi amesema mkoa umepoteza mtu muhimu pamoja na kwamba amefanya kazi muda mfupi lakini alikuwa ni mtu anyejituma katika kazi, huku kaimu kamanda wa polisi mkoani Singida SSP Mayala Towo akieleza jinsi marehemu alivyokuwa tayari kuwafundisha askari wengine bila kujali vyeo vyao.
Awali akisoma wasifu wa marehemu asp nyangi choma amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo na kumpelekwa hospitali ya makiungu mkoani singida ,hospitali ya jeshila polisi na hospitali ya muhimbili ,lakini juhudi nzuri za madaktari kuokoa maisha yake zilishindikana.
Akitoa salamu za mkuu wa jeshi ya polisi Tanzania IGP Ernest Mangu, kamishina mwandamizi msaidizi ambaye ni kamanda wa kikosi cha afya wa jeshi la polisi Tanzania SACP Paul Kasabago, pomoja na kutoa pole kwa mkoa amesema jeshi limepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akijituma katika kazi za jeshi la polisi.
Marehemu SACP Peter Kakamba amefanya kazi kama kamanda wa polisi mkoa wa Singida kwa muda wa miezi minne, uongozi wa mkoa wa Singida na baadhi ya wafanyakazi wameungana kwenda kwenye maziko yatakayo tarajia kufanyika tarehe mbili Desemba mkoani Katavi
