Habari Muhimu Kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Nchimbi


Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi ametoa wito kwa watumishi wa Umma Mkoani humo kuingia mwaka 2017 wakiwa na uelewa sahihi wa malengo ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kwa uweledi na kutatua matatizo yao kwa kasi ili kuinua maisha ya wananchi na Maendeleo ya Mkoa huo.

Mwaka 2017,tunataka tupige hatua kubwa zaidi kupitia raslimali zetu ambazo zitawezesha maendeleo katika Mifugo, Ukulima Mazao ya Kisasa, Ufugaji Nyuki, Ufugaji Samaki, Uvunaji wa Maji ya Mvua, Utunzaji wa Mazingira na Usindikaji wa Mazao kwa malengo ya ujumla ya kumuendeleza mwananchi na kutosheleza mahitaji ya Wanasingida na Soko la Dodoma Makao Makuu ya Nchi. Tunafanikiwa iwapo wananchi wote, watendaji na Viongozi wote tutashirikiana na kuwajibika kwa uwaminifu, uwadilifu na uweledi. Aliongeza Dr Nchimbi

Dkt Nchimbi amewataka wanchi wote wa Mkoani Singida washerekee Mwaka Mpya kwa amani bila kufanya mambo yeyote yatakayo ashiria uvunjifu wa amani ili kuufanya Mkoa huo kuwa ni kielelezo cha Utulivyo na amani na kuwafanya wageni wanaoingia Singida wasiwe na hufu na masha juu ya usalama wao.

Nawashauri wananchi wa Mkoa wangu wa Singida kuukaribisha mwaka mpya kwa kwenda kwenye nyumba za ibada na kumshukuru Mungu kwa Uzima aliotupatia na pia kuombea Mkoa wetu wetu na Nchi kwa ujumla ili Mungu azidi kutukirimia neema zake, kwa wale watakao jaribu kuleta fujo napenda kuwaambia kuwa Jicho na Sikio la Serikali hapa Singida liko makini na watashughulikiwa kikamilifu. Alimalizia Mh Dr Nchimbi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo