Na Lauden Mwambona, Mwananchi Mbeya.
Gari la Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi limeua mtoto aliyekuwa akivuka kwenye kivuko cha watembea kwa miguu eneo la Iyunga jijini hapa asubuhi ya leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Dhahiri Kidavashari amesema mtoto huyo, Recho Lutumo (15) baada ya kugongwa alipelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya ambako alikata roho.
Wakati ajali hiyo inatokea mbunge huyo alikuwamo kwenye gari hilo lililokuwa linaendeshwa na dereva wake, Gabriel Andrew (43) ambaye anashikiliwa na polisi.
