Wananchi wa kijiji cha Tandala kata ya Tandala
wilayani Makete mkoani Njombe kwa pamoja wamekataa kuendelea kutoa michango ya
shughuli za maendeleo kijijini hapo inayokatiwa risiti za vitabu vinavyonuliwa
katika steshenari badala yake wanataka vitabu vyote vitoke halmashauri.
Hayo yameibuliwa kwenye mkutano wa kijiji
hicho uliofanyika kijijini hapo hivi karibuni baada ya wanachi kuhoji risiti zitolewazo kuwa
sio halali na kusema kuwa hawako tayari kuendelea kutoa michango endapo
watapewa risiti hizo badala yake Afisa mtendaji wa kijiji afuate vitabi vya
mapato halmashauri
Afisa mtendaji wa kijiji cha Tandala Bw Ambele
Sanga amekiri kuwepo ukosefu wa risiti kutoka kwenye vitabu vitolewavyo
halmashauri na kuwataka wananchi hao kuwa wavumilivu wakati anafatilia vitabu
hivyo.
Pia wananchi hao wamezungumzia suala la mbolea za
ruzuku huku wakidai kuwa mbolea zinafika baada ya wananchi kupanda mazao yao.
Kwa upande wake kaimu afisa kilimo kijiji cha
Tandala Bw, Bruno Mwiche amewashauri wananchi hao kununua pembejeo hizo hata
kwa mwaka ujao.
Na Asukile Mwalwembe
Unaweza sikiliza sauti zote za tukio hilo hapa chini