Serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa
kuhakikisha umeme wa gridi ya taifa unaotumika ndani ya wilaya ya Makete
unatoka ndani ya Mkoa wa Njombe badala ya Mbeya ili kuepuka adha ya umeme huo
inayowakumba wananchi endapo matatizo yanajitokeza kwa mkoa wa Mbeya
Kauli hiyo imetolewa Mkoani Njombe na mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa katika kikao cha RCC mkoa
ambapo amesema wananchi wa Makete mara nyingi wamekuwa wakikosa huduma ya umeme
mara kwa mara kutokana na matataizo yanayojitokeza kwenye miundombinu ya
TANESCO Mkoa wa Mbeya hivyo utatuzi wake umekuwa Mgumu kutekelezeka kwa wakati
Kisha Mh Mtawa akatoa pendekezo kwa serikali ni
nini kifanyike ili kuondoa changamoto hiyo inayowakabili wananchi wa Makete wanaotegemea
umeme wa gridi ya taifa
Katika hatua nyingine kupitia kwa mwenyekiti huyo
halmashauri ya wilaya ya Makete imelalamikia gharama kubwa za matengenezo ya
magari zinazotozwa na wakala wa serikali TEMESA, ambapo halmashauri hiyo magari
iliyokuwa ikilipia shilingi laki 8 kwa matengenezo kwa sasa wanalazimika
kulipia ZAIDI ya milioni 3 kwa TEMESA
Hali hiyo ikamlazimu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Njombe Dkt Rehema Nchimbi kutaka maelezo ya suala hilo kutoka TEMESA
Majibu hayo
yakapelekea aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi ambaye
kwa sasa amehamishiwa mkoa wa Singida kutoa kauli kuhusiana na hilo
Sikiliza sauti hizi hapa chini