Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Makete mkoani Njombe zimeendelea kuleta usumbufu katika Barabara ya Makete Njombe, baada ya kifusi kilichorundikwa barabarani kugeuka tope hali iliyopelekea Magari Kukwama. Picha zote zinaonesha magari yaliyokwama kijiji cha Ikonda njia panda ya kuelekea hospitali ya Consolata Ikonda leo asubuhi
Jitihada za kulivuta basi la Japanese lililokwama, Basi hilo linafanya safari zake kati ya Makete Njombe
Trekta likiwa limekwama
Jitihada za kulinasua basi hilo zikiendelea
Hali halisi ndiyo hiyo wadau
Trekta nalo likivutwa
Abiria wakiingia kwenye basi safari iendelee