Akatwa sikio baada ya kufumaniwa na Mke wa Mtu

Dereva bodaboda wa mji mdogo wa Qatesh Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, amejeruhiwa kwa kukatwa sikio kwa kutumia kisu, baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa dereva wa teksi.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Francis Massawe amesema tukio hilo lilitokea Desemba 21 saa 6.10 usiku kwenye kitongoji cha Qendangonyi, kata ya Ganana wilayani Hanang’.


Kamanda Massawe alimtaja dereva bodaboda huyo kuwa ni Emmanuel Dani (30) mkazi wa eneo hilo la Qendangonyi, akidaiwa kufumaniwa na mke wa dereva teksi Heavenlight Kimro (40) ambaye naye ni mkazi wa kitongoji hicho.


Massawe amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu w mapenzi na muathirika amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa na wanamshikilia mtuhumiwa huo kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo