Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiingie katika matukio ya kihalifu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi, Mbande Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumza Jumanne hii katika uzinduzi wa madarasa nane ya shule ya msingi Mbande Temeke jijini Dar es salaam, Makonda amesema mtoto yeyote aliyechini ya miaka 17 atakaye kamatwa kwa tuhuma za uhalifu, na wazazi wa mtoto huyo atakamatwa.
Makonda akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Mbande
“Mtoto wa umri wa miaka 17 akikamatwa kwa kosa la uhalifu, uvamizi au akikamatwa kwa makosa ya uporaji au panya road nimewaambia polisi na wazazi wao akamatwe. Mtoto ni wakwako unatakiwa kuangalia muenendo wa mtoto wako, kwahiyo wazazi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao,” Makonda aliiwaambia wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya Mbande.
RC Makonda amewataka wazazi hao kuwahimiza watoto wao kusoma pamoja na kufuatilia maendeleo yao ya kila siku.