Waandamana mpaka Wizarani na kuelezea Mateso wanayopata kwa Kukosa Mikopo

Wanafunzi zaidi ya mia tano wa fani mbalimbali kutoka chuo cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam waliokosa mikopo wamekusanyika wizara ya elimu sayansi na teknolojia kwa lengo la kupata kauli ya serikali juu ya hatima yao huku wakihoji uhalali wa vyuo vingine kupata mikopo kwa asilimia 80 lakini wao ni asilimia tano tu.

Wakizungumza wizarani hapo baadhi ya wanafunzi hao wamedai kuwa licha ya kuishi mazingira magumu pia hawawezi kujilipia ada ambayo ni zaidi ya milioni sita na kwamba wanashangazwa na kitendo cha bodi ya mikopo awali kuorodhesha kuwa wapo kwenye orodha ya wanaostahili kupata mkopo lakini baadaye wakawaondoa.

Serikali licha ya kuwataka kufuata utaratibu wa kuwasilisha madai yao imewaeleza kuwa wanaostahili kupata mkopo ni watoto yatima ambao hawana baba wala mama na kuwaahidi kwenda kuzungumza nao huko chuoni ili kuona namna ya kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo wanafunzi hao wameelza kutokuridhishwa na majibu ya serikali kwa madai kuwa serikali iliahidi kuwa itatoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili hasa ambao wazazi hawana uwezo.

Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi lililazamika kuimarisha ulinzi katika jengo la wizara hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo