Makubwa...Walimu waacha Kufundisha na Kujikita Kwenye Bodaboda

Sababu za mkoa wa Morogoro kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu zimetajwa kuwa ni waalimu kujihusisha na masuala ya siasa na kazi za bodaboda na kuacha ufundishaji pamoja na wanafunzi kuendekeza ngoma za asili ambapo miongoni mwa shule 10 za mwisho, tano ni za mkoa wa Morogoro.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa mkoa wa Morogoro,ambapo wilaya ya Morogoro imeshika nafasi ya mwisho katika ufaulu, na kutoa shule tano kati ya 10 zilizoshika mkia kitaifa, katibu tawala mkoa wa Morogoro Dkt. John Ndunguru amesema baadhi ya walimu wamebainika kujihusisha na siasa na kusahau ufundishaji hivyo kuagiza watakaobainika wafukuzwe kazi, huku sababu nyingine zilizoshusha ufaulu akitaja kuwa ni walimu kujiingiza kwenye biashara ya  bodaboda,wazazi na walezi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao,shule za pembezoni walimu kutoripoti na ngoma za asili na vigodoro.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Sudi Mpili amesema jiografia ya wilaya hiyo na miundombinu duni vinechangia baadhi ya shule kushindwa kufikika kiurahisi lakini wameweka mikakati kuboresha elimu huku mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly akitaja changamoto nyingine ya uhaba wa nyumba za walimu imefanya walimu wengi kushindwa kukaa jirani na shule hivyo wengi kushindwa kuripoti na shule kukabiliwa na uhaba wa walimu.

Kwa mujibu wa katibu tawala msaidizi upande wa elimu mkoa wa Morogoro,Wariambora Nkya,jumla ya wanafunzi 44,212 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu na 25,846 wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, july wanafunzi 293 wakishindwa kufanya mtihani wakiwemo mabinti 20 kutokana na kupata ujauzito.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo