CCM Yaomba Serikali Kulinda Maisha ya Diwani wa CHADEMA Aliyehamia CCM

Kufutia diwani machachari wa kata ya Tanga  Songea  mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chadema Bw.Mussa Ndomba kurudi CCM na kuwaacha wananchi wake njia panda bila uwakilishi,wananchi wake wamesikitikia hatua hiyo.

Wakati akirejesha kadi yake  ya CHADEMA kwenye ofisi za CCM mkoa wa Ruvuma Bw.Mussa Ndomba ametaja sababu mbalimbali za kujitoa  kwenye chama hicho ikiwemo kutishiwa maisha yake  na makundi yanayopingana kwenye chama cha Demokrasia na maendeleo Ruvuma  na kukiukwa kwa katiba ya CHADEMA katika kufanya maamuzi na uteuzi wa viti Maalum.

Wakati wana CCM wakifurahia hatua ya Bw.Mussa Ndomba kwenda CCM wakazi wa kata ya  Tanga wamesikitishwa na hatua hiyo kwa kuwa watakosa uwakilishi kwa muda.

Akimpokea Bw.Ndomba Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Bw Oddo Mwisho ameiomba serikali kumuhakikishia usalama wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo