Mahakama kuu Yawafutia Kifungo wanajeshi wawili wa JWTZ

Mahakama kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es Salaam,imetengua hukumu ya kifungo cha miaka 3 dhidi ya askari wawili wa Jeshi la wananchi JWTZ iliyotolewa na Mahakaka kuu ya kijeshi (JWTZ) na kuamuru kuwaachia huru askari hao.

Wakitoa hukumu hiyo jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti jaji kiongozi, Fedinand Wambari akisaidiana na Jaji Sekiet Kihio na Ama-Isario Munisi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhusu rufani ya walalamikaji dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG),Jaji Munisi amesema Mahakama hiyo inatengua hukumu ya kifungo cha miaka mitatu kwa wanajeshi hao kutokana mapungufu ya kisheria katika mwenendo wa kesi hiyo wakati wa usikilizwaji watuhumiwa hao hawakupata nafasi ya kuhojiana baada ya ushahidi wa utetezi wao.

Wakili wa washtakiwa hao Bwana Rwegasira ameiomba Mahakama kufuta mwenendo wa hukumu iliyotolewa na Mahakama ya kijeshi kwa mshtakiwa wa pili kutokana na makosa yaliyokuwa yanawabili kuwa sawa na makosa yaliyofutwa kwa mashtakiwa wa kwanza hatua ambayo jopo hilo lilikubali.

Akijibu hoja za walalamikaji,wakili wa Jeshi la wananchi jwtz,Meja Godwill Benda amesema kutenguliwa hukumu dhidi ya mshtakiwa wa kwanza Mahakama imefuta mwenendo na hukumu ya awali na kwamba kesi dhidi ya mlalamikaji wa pili haina mashiko kisheria ambapo ameiomba mahakama hii ijielekeze kutoa amri kama iliyotolewa kwa mlalamikaji wa kwanza inayoruhusu ufunguliwaji upya wa mashtaka mengine.

Mahakama hiyo imewaachia baada ya kusikiliza rufani iliyokatwa na askari mt 64781 sajenti theodory kija na mt 57209 sajenti dai chiro waliohukumia kifingo cha miaka mitatu na mahakama ya kijeshi baada ya kukutwa na hatia ya vitendo vya kuharibu murua na taratibu za kijeshi na kupatikana na  makosa sita ikiwamo kughushi nyaraka,mihuri,vitendo vya kuharibu murua na taratibu za kijeshi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo