Lema amharibia waziri Simbachawene Bungeni

GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amesema kwamba, alishauriwa na George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa, amfungie ofisini Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ili kuibua vurugu na kisha (Simbachawene) aingilie.
Akizungumza bungeni leo asubuhi, Lema amesema Simbachawene alimtaka yeye na viongozi wengine wa Chadema wamfanyie vurugu mkurugenzi huyo kisha tukio hilo lioneshwe katika Runinga ili waziri aingilie kati mgogoro huo kwa madai, utakuwa umedhihirika.
“Nilimwambia Waziri Simbachawene kuwa Arusha tuna tatizo kwenye halmashauri tunaomba msaada, akanishauri tukafanye fujo ili aone kwenye vyombo vya habari na apate nafasi ya kuingilia mgogoro huo kwasababu rais amewapa nguvu wakuu wa mikoa.
“Akaniambia siwezi kuja kichwa kichwa nenda kafanye fujo, mfungieni mkurugenzi nje halafu mimi nione kwenye TV ili niingilie mgogoro huo. Yaani waziri anaogopa kuingilia migogoro katika halmashauri,” ameeleza Lema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo