Mradi wa maji wanaodai wananchi hao kuwa ulichakachuliwa kwa kuwekewa mabomba feki
Mambomba yaliyofukiwa yakivujisha maji ilihali ni mapya
Mwenyekiti wa kijiji cha Ndulamo Bw Tweve akiongoza mkutano huo na wananchi
Kutokana na tatizo la maji linalokikabili kijiji cha Ndulamo kata ya Iwawa
wilayani Makete mkoani Njombe, uongozi wa kijiji hicho umelazimika kuitisha
mkutano wa dharura wa kuipatia ufumbuzi kero hiyo ya maji
Katika mkutano huo wa dharura ulioitishwa jana kijijini hapo wananchi hao
wamelazimika kukubali kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa kijiji uliopo jirani na
zahanati ya kijiji chao ili fedha zitatazopatikana zitumike kununulia mabomba ili kuondoa
tatizo hilo la maji
Baadhi ya wananchi waliozungumza mkutanoni hapo wamepewa nafasi ya kutoa
maoni yao kabla ya kutoka na maazimio ya pamoja ambapo wamesema wamechoshwa na tatizo hilo ambalo linakaribia kufikia mwaka mmoja lakini wakiendelea kuteseka kutembea umbali mrefu kufuata maji mtoni na kwenye vidimbwi
Katika mkutano huo Afisa mtendaji wa kijiji hicho Majuto Mbwilo akatolea
ufafanuzi zaidi wa suala hilo la maji kijijini hapo kwa kueleza sababu
zilizopelekea tatizo hilo kuwepo kuwa ni mradi wa TASAF wa miaka iliyopita (2013) kuwapelekea mabomba yaliyopo chini ya kiwango ambayo kwa sasa yamepasuka na
yanavujisha maji na kila yanapokarabatiwa hasa kwenye viungo bado yanaendelea kupasuka
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Lilio Tweve ndiye aliyeongoza mkutano huo na
baada ya majadiliano ya muda mrefu na wananchi, wakakubaliana kuuza kwa mnada
msitu wa kijiji hicho Jumamosi ya wiki hii na fedha zitakazopatikana zielekezwe
kwenye kumaliza kero hiyo ya maji, na akatangaza maazimio ya mkutano huo
kuhusu maji mbele ya waanchi wote
Unaweza kusikiliza sauti za Mkutano huo kwa kubofya hapa chini