Katika kuhakikisha stendi mpya ya Tandala katika wilaya ya Makete mkoani
Njombe inaendelea kutumiwa na vyombo vya usafiri pongezi zimetolewa kwa
wamiliki wa vyomo vya usafiri hususan Mabasi ya abiria kwa kuanza kuitumia
stendi hiyo.
Akizungumza nasi Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw Andowisye
Memba ametoa pongezi hizo kwa kusema kuwa ushirikiano wanaoutoa ni mzuri na
kuwataka wasafiri kutambua kuwa kwa sasa stendi iliyopo katika kitongoji cha
Singida, ndiyo inayotambulika rasmi na inaendelea kufanya kazi.
Aidha amewatoa wasiwasi abiria watakaoshukia katika stendi hiyo Kwa kusema
kuwa watapata usafiri mwingine wa pikipiki hivyo waendelee kuitumia stendi
hiyo.
Pia ameongeza kuwa kwa sasa hawatatumia kituo kingine kushusha abiria mbali na stendi mpya ya Tandala.
na Asukile Mwalwembe
sikiliza sauti hapo chini kwa kubofya play