DC RUTH MSAFIRI AKIKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA HIYO NI BARABARA YA LIMA LORE UREFU WA KILOMITA 14.5 kulia wa kwanza dc wilaya ya njombe Ruth Msafiri na wa pili mkurugenzi Monica kwiluhya.
Watendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wametupiwa lawama kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye fedha za mapato wanazokusanya hasa kwenye ushuru wa mbao na mazao.
Hayo yameibuka leo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha Kuwasilisha tarifa za kwenye kata ambapo mwenyekiti wa kamati ya uchumi ambaye pia ni diwani wa kata ya Kidegembiye Julius Salingwa amesema kuwa mapato yameanza kushuka na kwamba kuna dalilili za mgomo baridi kwa baadhi yao
Ushuru katika halmashauri ya wilaya ya njombe tofauti na ilivyo katika maeneo mengine hukusanywa kwa kupitia wataalamu mbalimbambali wa halmashauri ngazi ya kata ambapo katika siku chache zilizopita imedaiwa kuwa mapato yalionekana kuongezeka lakini kwa sasa yameanza kuporomoka
Viongozi wa ngazi ya juu ya halmashauri hiyo akiwemo mwenyekiti mkurugenzi na madiwani na Baadhi ya wakuu wa idara wamefanya doria na kukuta magari yanayosafirisha mbao pasipo kulipa ushuru kama sheria inavyoelekeza
Kwa upande wao baadhi ya watendaji wa kata wamesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazo wakabili katika kufanikisha ukusaji wa mapato ni pamoja na baadhi ya wafanyabiashara waio waaminifu kufanya kazi usiku wa manane ,kukosa ulinzi na baadhi yao kutojua namna ya kutumia mashine za EFD
Na Patrick Mfugal