Waendesha bodaboda zaidi ya mia tatu kutoka ukonga jijini dsm wamenadamana hadi katika ofisi ya mtendaji kata katika kata ya Ukonga kupinga kile wanachodai kuwa vitendo vya uonevu na manyanyaso wanayodaiwa kufanyiwa na baadhi ya askari pamoja na vijana wa ulinzi shirikishi wakati wakiwakamata.
Wakizungumza kupitia kituo cha Chanel Ten viongozi wa bodaboda hao wamesema wamekuwa wakikamatwa kwa nguvu na baadae kutozwa fedha nyingi zaidi ya laki moja na nusu bila kupewa stakabadhi au risiti na kumtaka kamanda wa polisi kanda Maalum Simon Siro kuwachunguza askari wake wanaodaiwa kufanya hivyo.
Aidha vijana hao wa boda boda wamelalamikia kufungwa kwa njia waliyokuwa wakitumia na shirika la reli TRL kwa madai kuwa wamekuwa wakiharibu eneo hilo kwa kupitisha pikipiki eneo hilo.