YAH: KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA
KIJAMII IKIMNUKUU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS
(MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA)
MHESHIMIWA ANGELLAH J. KAIRUKI (MB), KUWA SERIKALI
ITAANZA KUTOA AJIRA, KUPANDISHA VYEO NA KULIPA STAHIKI
MBALIMBALI ZA WATUMISHI WA UMMA MWEZI FEBRUARI, 2017.
1. Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu
Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza
kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi
wa Umma mwezi Februari, 2017.
Chanzo cha habari hiyo ni mtandao
wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JFExpert
Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.
2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla
kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha
Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla
wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama
kawaida.
3. Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo
litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha
2
2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na
Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa
Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka
husika.
5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya
kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika
kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.
Imetolewa na:
Florence Temba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
24 Oktoba, 2016
SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUWA ITAANZA KUTOA AJIRA by Ahmad Issa Michuzi on Scribd