Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aongelea Changamoto hizi Zilizomkumba

Mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Saalam na rais mstaafu wa awamu ya nne, Mh Jakaya Kikwete ameelezea changamoto alizozikuta chuoni hapo baada ya kuteuliwa na rais Magufuli ikiwemo mikopo, hosteli, maktaba na miundombinu mibovu ya chuo kutokana na ukongwe wake huku akielezea namna anavyokabiliana nazo kuzitatua.

Akizungumza katika kongamano la miaka 55 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho Mh Kikwete amesema katika kipindi chake cha ukuu wa chuo atahakikisha anaunganisha uongozi wa chuo na wadau mbalimbali ikiwamo serikali ili wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho ambao hawana uwezo wa kujisomesha waweze kupata mikopo ili waweze kuendelea na masomo.

Makamu mkuu wa chuo hicho Prof Rwekaza Mukandara akielezea historia ya chuo hicho amesema tangu kilipoanzishwa mbali na kutoa elimu bora kwa wanafunzi pia kimetoa viongozi wengi wa ngazi za juu na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza chuoni hapo wataweza kwenda kufanya utafiti ndani na nje ya nchi.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1963 kikiwa na wanafunzi 14 walimu sita ambao walikuwa wakisoma katika majengo ya chama cha mapinduzi CCM Lumumba na baadae kuhamishiwa eneo la mlimani ambapo lengo la kuanzishwa kwake ni mikakati ya kuleta ukombozi katika nchi za Afrika na kwa sasa kina wanafunzi zaidi ya 24,000. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo