Tanzania na Morocco zimesaini mikataba 21 ya makubaliano kushirikiana katika masuala mbalimbali kwa lengo la kuboresha uchumi wa mataifa hayo mawili.
Akizungumza baada ya kuweka saini mikataba hiyo rais Dkt. John Magufuli amesema makubaliano hayo ni mwelekeo mzuri wa kujenga Tanzania mpya katika uchumi wa viwanda huku akiwahakikishia wawekezaji kutoka Morocco kuwa nchi ya Tanzania ni nchi ya amani
“Kwahiyo makubaliano haya ni mwelekeo mzuri wa Tanzania mpya ambayo tumepanga katika kujenga uchumi wetu uweze kukua kwa asilimia 7.2 ifikapo mwishoni mwa mwaka, na mwelekeo umeanza kuonyesha hivyo kwasababu katika robo ya pili ya mwaka huu uchumi wetu umekuwa kwa asilimia 7.9 na infletion imeanza kushuka karibu asilimia 7 sasa hivi infletion imefikia 4.5 percent,”alisema Rais Magufuli.
“Kwahiyo niwahakikishie wenzetu kutoka Morocco tuko kwaajili ya kujenga uchumi wa kisasa. Kwahiyo naweza kuwathibitishia hili ni eneo zuri la kuweka uwekezaji,”alisisitiza.