Mkurugenzi ampigisha deki Mwalimu Mbele ya wanafunzi

Moja ya habari kubwa iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii kutoka gazeti la Tanzania Daaima yenye kichwa cha habari ‘Mkurugenzi ampigisha deki mwalimu’
Habari kutoka gazeti la Tanzania Daima imedai kuwa jana October 21 2016 mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliud Mwaiteleke ameingia kwenye kundi la wakurugenzi wanaowanyanyasa na kudhalilisha watumishi wa chini baada ya kudaiwa kumuamuru mwalimu wa shule ya sekondari ya Shilala, Hamis Sengo, kudeki darasa zima, mbele ya wanafunzi wake.
Inaelezwa kuwa mkurugenzi huyo alifika shuleni hapo akiwa na watendaji wengine wa wilaya na kukuta madarasa yakiwa machafu, ndipo aliamuru  mwalimu huyo kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, jambo ambalo limepingwa vikali na kulaaniwa na chama cha walimu ‘CWT’ wilayani humo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo