Breaking News: Mbunge Wa Makete Ajitokeza, Aeleza kama Kalamba Mshahara Hewa (AUDIO)

Mbunge wa jimbo la Makete mh. Prof. Norman Sigala King amekanusha tuhuma zilizotangazwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Dhidi yake kuwa alikuwa bado akipokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa muda wa miezi mitano baada ya kuchanguliwa kuwa mbunge.

Amesema hayo leo hii wakati akizungumza na kituo cha 91.5 Green FM katika mahojiano Maalum na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuwa serikali hii ya awamu ya tano ipo makini haiwezi kuingiza mshahara huo wa ukuu wa wilaya katika akaunti yake wakati ikijua kuwa yeye ni mbunge kwa sasa.



Mh. Norman pia ametoa wito kwa vyombo vya habari kutotangaza taarifa hiyo bila kumhoji ili kuthibitisha tuhuma hizo huku akiwataka wananchi wa Makete kuendelea kufanya kazi ili kuijenga Makete na kuwa yeye kama mbunge wao yuko makini.

Pia Mbunge huyo amesema hakuhojiwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi kama lilivyoandika na tayari ameshafika kwenye ofisi za Gazeti hilo kwa hatua zaidi

Bonyeza play hapo chini Kusikiliza mahojiano hayo kwa njia ya sauti:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo