Polisi wadai ‘Bado tunamtafuta Masanja Mkandamizaji’

August 17 2016 Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imewahoji wasanii wanne wa kundi la sanaa ya uigizaji Orijino komedi akiwemo meneja wao Seki kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.

kwa mujibu wa tovuti Millardayo imempata kwenye exclusive interview kaimu kamishna wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Hezron Gyimbi ambaye amesema hadi sasa bado wanamtafuta Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.

Wamekamatwa jana saa 10 jioni ambapo wamehojiwa na wamekaguliwa sehemu wanazokaa kuona kama wana vitu zaidi ya uniform‘-Hezron Gyimbi 

Tunakamilisha hatua za kiupelelezi, makosa yanadhaminika wakipata watu wanaweza wakawadhamini sababu dhamana ni haki ya mtu‘-Hezron Gyimbi

Jalada kesi ya wasanii orijinal komedi linaandaliwa litapelekwa kwa DPP, ndio mwenye dhamana ya kupeleka mahakamani‘-Hezron Gyimbi

Bado tunamtafuta Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ kwa sababu yule atakuwa shahidi muhimu sana kwetu;-Hezron Gyimbi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo