Mkazi wa Kijiji cha Nyisense wilayani
Serengeti Mkoa wa Mara, Matiko Nyamanche (28) ameuawa kwa kupigwa na
wananchi kwa tuhuma za wizi wa kifaranga cha kuku chenye thamani ya
shilingi 1500.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,
Ramadhani Ng’azi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12 mwaka
huu majira ya saa nne usiku.
Kamanda Ng’azi alisema siku ya tukio kundi la wananchi walimshambulia Nyamanche kwa silaha za jadi baada ya kutuhumiwa kuiba kifaranga cha kuku na mifugo mali ya Machele Mtatiro.
Kamanda Ng’azi alisema siku ya tukio kundi la wananchi walimshambulia Nyamanche kwa silaha za jadi baada ya kutuhumiwa kuiba kifaranga cha kuku na mifugo mali ya Machele Mtatiro.
Alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali
Ng’azi aliongeza kuwa watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.
Ng’azi aliongeza kuwa watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Senta, Ryoba
Tamanya alisema kabla ya kukutwa na umauti Nyamanche alikuwa anakunywa
pombe na wenzake na wakati anarudi alipita kwa shemeji yake Makere
Mtatiro na kuiba kifaranga hicho na kukimbia.