Mkuu wa Wilaya apewa Maagizo 6

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo  amemuapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kisarawe,  Happyness William huku akimpa maagizo sita  kwenda kutekeleza katika kuwatumikia wananchi kwenye utumishi wake.

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, imeambatana na kuapishwa kwa wajumbe  wawili wa baraza la ardhi la Wilaya ya Kibaha. 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wakuu wa wilaya za mkoa huo ambao waliapishwa Januari Mosi  mwaka huu pamoja na watumishi wa idara mbalimbali ndani ya Mkoa wa Pwani.

Maagizo aliyopewa Mkuu huyo wa Wilaya ni kusimamia suala la ulinzi na usalama, kilimo cha ufuta korosho na mihogo, kuongeza kasi ya urasimishaji wa ardhi, kusimamia uwekezaji wa viwanda na kutatua migogoro ya ardhi iliyomo wilayani humo.

“Mbali na maagizo hayo yote pia nakusisitiza uende ukasimamie  Ilani ya Uchaguzi  ya Chama cha  Mapinduzi ambayo kimsingi inasisitiza utawala bora, usije ukaenda kufanya kinyume na hayo maana ukienda kinyume utakuwa umekiuka maagizo ya Serikali na utumishi wako utakuwa mgumu,” amesema.

Pia, alimtaka Mkuu huyo wa Wilaya kwenda kuendeleza mapambano dhidi ya watumishi hewa kwa kushirikiana na idara mbalimbali, huku akimsisitiza kuweka mbinu na mipango ambayo itafanikisha kuongenza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo