Mama azuiwa kutoka wodini baada ya kujifungua watoto watatu kwa Mpigo

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imedaiwa kumzuia kutoka wodini Lucy Samson (25) aliyejifungua kwa upasuaji watoto watatu tangu Agosti 24 mwaka huu, ikimdai Sh375,540. 

Madai hayo yamekuja licha ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kutoa agizo la kutowatoza fedha wajawazito 

Akitoa agizo hilo Agosti 22 wakati akielezea kuhusu mapitio ya Sera ya Afya ya mwaka 2007, Mwalimu alipiga marufuku kuwatoza fedha wajawazito, watoto chini ya umri wa miaka mitano na wazee wasiojiweza huku akisema atamchukulia hatua mganga mkuu yeyote wa mkoa au mfawidhi atakayekiuka agizo hilo. 

Lucy amesema alilazwa tangu Julai 24 kabla ya kujifungua lakini amezuiwa kwa kushindwa kulipa deni hilo. 

Alipotafutwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kutoa ufafanuzi kuhusu mgonjwa huyo, hakupatikana na simu yake iliita bila kupokewa na baadaye ilikuwa inaita na kukata.

chanzo:mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo