Mbunge
wa Ubungo, Saed Kubenea Jumatatu ya Agosti, 15 amefika katika ofisi za
Jeshi la Polisi kanda ya kati kufanyiwa mahoajiano kwa madai ya kuandika
makala ya uchochezi katika gazeti la Mwanahalisi,
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu jambo hlo, Mwanasheria wa Chadema ambaye
aliambatana na Kubenea kituoni hapo, Tundu Lissu alisema Kubenea alipewa
taarifa kuwa anatakiwa kufika kituo hicho kwa ajili ya kufanyiwa
mahojiano.
Alisema
baada ya kufika kituoni hapo, Kubenea alihojiwaa kwa kipindi
kisichozidi masaa mawili na akituhumiwa kwa kuandika makala ya uchochezi
katika gazeti la Mwanahalisi iliyochapishwa kati ya Julai, 25-30.
“Aliitwa
kuhojiwa kuhusu makala aliyoandika kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu
uwa makala hiyo ni ya kichochezi na kutaka kujua kama kweli alizungumza
na watu ambao wanasema waliteswa au kubalance habari kwaa upande wa
Polisi lakini ukiangalia maswali yote yana majibu ndani ya hiyo makala,”
alisema Lissu.
Aidha
alisema kuwa katika mahoajiano hayo hapakuwa na mazungumzo kuhusu
kufungiwa kwa gazeti la Mseto na amepewa dhamana ya kuwa nje na kutakiwa
kurejea kituoni hapo Alhamisi ya wiki ijayo ili kujua kama Polisi
watapeleka mashtaka mahakamani au wataacha.