Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE
iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora).
Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi
Asha D. Abinallah na Mshauri wa Miradi Bw. Ericus Kimasha.
Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.
Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.
Jamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole
Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajaliTimu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.
Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.
JamiiForums