Habari tulizozipata usiku huu wa Agosti
23, 2016 ni kuhusu kuuawa kwa askari polisi kufuatia tukio la uporaji
lililotokea katika bank ya CRDB tawi la Mbande, Mbagala jijini Dar es
salaam.
Wanaodaiwa kufariki dunia ni E5761 CPL YAHAYA,F4660 CPL HATIBU na G9544 PC TTITO.
Inasemekana majambazi wameondoka na SMG moja.
Inadaiwa kuwa tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo na kwamba mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.
Taarifa zinasema kuwa majambazi hayakuingia ndani ya bank.
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hili>> "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi"