skip to main |
skip to sidebar
Wananchi Wajitolea kutengeneza barabara kwa majembe ya mikono
Wananchi wa mtaaa wa Ruhuwoiko kisiwani manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
wameamua kutengeneza barabara kwa majembe ya mikono kwa kung’oa miti
baada ya manispaa kuzitelekeza barabara za mitaa kwa miaka mingi bila
kuzitengeneza.kutoka Songea tupate taarifa Zaidi.
blog hii imeshuhudia wananchi hao wake kwa waume wakikata miti na
kuiondoa wamesema wamejitolea kutengeneza barabara kwa nguvu zao
kutokana na mtaa huo kukosa barabara za kupita gari na kwamba wamechoka
kuitwa mtaa wa mazagazaga usio na miundombinu maji na barabara.
Kutokana jitihada na majitoleo ya wananchi diwani wa kata ya Ruhuwiko
Wilbert Mahundi amesema baada ya wananchi kujitolea nguvu zao
atahakikisha kupitia kiasi kidogo cha fedha zlizootolewa na manispaa kwa
ajili ya miradi ya maendeleo ya kata ya Ruhuwiko anapeleka katapila la
kukwangua barabara mapema iwezekanavyo.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi