Wanafunzi 430 kati ya 510 wa Shule ya Msingi Kabasharo, Kijiji cha Kyota wilayani hapa Mkoa wa Kagera, wanasomea kwenye viwanja vya kupumzikia kutokana na kukosa madarasa.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo iliyoanzishwa miaka tisa iliyopita,Papias Anthony alisema ina madarasa mawili yaliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Mwalimu Anthony alisema licha ya kusomea uwanjani, wanafunzi hao hukatisha masomo mvua inaponyesha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyota, Daudi Kiluma alisema uongozi kwa kushirikiana na wananchi umepata Sh4.8 milioni zitakazotumika kujenga madarasa.