Kauli
hiyo imetolewa Jana na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kesi wakati
alipofika kijijini hapo kusikiliza kero za wananchi ikiwemo baada ya wao
kutangaza kugomea shughuli za maendeleo kwa madai ya kutoridhishwa na
mwenendo wa shauri la kuuawa mtoto mmoja kijijini hapo na watuhumiwa wa
mauaji hayo kupewa dhamana
Mh
Kesi amesema anaungana na wananchi hao kuwapa pole kwa msiba huo
uliowapata na kusema hoja zote zilizotolewa na wananchi katika mkutano
huo amezichukua na kuahidi kwenda kuzifanyia kazi na wananchi kuona
majibu kwa kuwa ziko hoja ambazo zipo ndani ya uwezo wake na nyingine
zilizopo kwa upande wa mahakama watashirikiana na wataalamu wakiwemo
wanasheria kuzitatua kisheria
Pia
mkuu huyo amelaani mauaji hayo na kusema si vizuri mtu yeyote
kujichukulia sheria mikononi na kusababisha kifo cha mwananchi yeyote
Aidha
mkuu huyo amewaagiza viongozi wa kijiji hicho na kata ya Ukwama kutenga
siku maalumu ya kusikiliza kero za wananchi ili zitatuliwe haraka
iwezekanavyo kwa kuwa njia hiyo itasaidia kuimarisha kijiji hicho na
kisonge mbele kimaendeleo
Katika
mkutano huo Mkuu wa wilaya ametoa nafasi ya kusikiliza maoni ya
wananchi kuhusiana na tukio la mauaji ya mtoto wa miaka 17 lililotokea
kijijini hapo miezi miwili iliyopita
Mwanasheria
wa wilaya ya Makete Bw. Godfrey Gogadi ametolea ufafanuzi wa baadhi ya
hoja za wananchi ikiwemo kutojadili suala ambalo lipo mahakamani kwa
kuwa sheria hairuhusu, na kwa kuwa suala la mauaji hayo lipo mahakamani
ni vema wananchi wakawa na subira na kuiachia mahakama itende haki, na
kwa kuwa malalamiko yao wameyafikisha kwa mkuu wa wilaya, atashirikiana
na wataalamu wake ili suala hilo lifikie mwisho vizuri bila kuathiri
chochote