Msafara wa waziri wa sheria na katiba Dr. Harrison Mwakyembe umepata ajali baada ya gari lililokua limembeba Mkurugenzi wa mashtaka na makosa ya jinai DPP Biswalo Mganga kupinduka katika kata ya Bwanga wilayani Chato wakitokea mkoani Geita.
Imedaiwa
chanzo cha ajali hiyo ni dereva kujaribu kuwakwepa watoto wawili
waliokuwa wakikatiza barabara ghafla, taarifa zinadai kuwa katika ajali
hiyo hakuna vifo wala majeruhi.
