Mzee Masevela Jela Miaka 32 kwa kubaka mtoto wa Miaka 12, Hapa kuna picha 10 na habari kamili











Mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemhukumu kwenda jela miaka 32 mkazi wa kijiji cha Kitula wilayani hapa kwa kosa la ubakaji na shambulio la aibu kwa mtoto mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la tano.

Bw.Edward Ahazi Masevela (54) mkazi wa Kitula kata ya Kipagalo wilayani Makete amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela kwa makosa mawili tofauti baada ya mahakama kuridhika na ushahidi pasipo shaka kuwa alimbaka mwanafunzi wa darasa la tano jina linahifadhiwa wa shule ya msingi Mahulu ambapo imedaiwa alitenda kosa hilo kati ya mwezi Julai 2015 hadi Aprili 2016.

Kabla ya hukumu kutolewa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ambaye ni Hakimu wa mkoa wa Njombe Bw.Cosmas Joseph Hemela alitoa nafasi ya kujitetea kwa mshtakiwa Bw.Edward Masevela ambapo katika utetezi wake ameomba mahakama imuone hana hatia kwani hakutenda kosa hilo lakini Mahakama imesema Mtuhumiwa badala ya kujitetea yeye mwenyewe amekuwa akitoa maneno ya kutuhumu ushahidi wa walalamikaji ambao ni watoto kwamba wamefundishwa.

Hakimu wa mkoa wa Njombe bw.Cosmas Hemela aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amesema mahakama imemkuta na hatia ya makosa mawili mtuhumiwa ambapo katika kosa la kwanza la ubakaji amehukumiwa miaka 30 jela na kosa la shambulio la aibu amehukumiwa miaka miwili jela na ameanza kutumikia adhabu zote mbili Julai mosi.

Hukumu hiyo kwa kosa la kwanza imetokana na kifungu cha 130 (1)(2)(e) na kifungu 131 (1)kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 amefungwa jela miaka 30, na kwa kosa la pili la shambulio la aibu linatoka kifungu 138 (1)(a) / (2)(b)kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 amefungwa miaka miwili.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifunguliwa Mei 10, 2016 kwa makosa mawili, moja likiwa la ubakaji na la pili ni shambaulio la aibu pamoja na hukumu hiyo Rufaa ipo wazi na Bw.Masevela anaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia Julai mosi.


Nje ya mahakama ya wilaya ya Makete baadhi ya wananchi ambao wamekataa kutaja majina yao wala kupigwa picha wameonesha kufurahishwa na hukumu hiyo kwa kusema mahakama imetenda haki, huku wengine wakisema hawaamini kama kweli ametenda makosa hayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo