Mwanafunzi Ujuni Makete Augua ghafla na Kufa, Uchawi watajwa (Audio)

Jamii wilayani Makete mkoani Njombe imeshauriwa kuondokana na imani potofu ambazo mara nyingi huzielekeza pindi kunapotokea kifo cha ghafla ambapo mara nyingi hukihusisha na imani za kishirikina

Kauli hiyo imetolewa kufuatia kifo cha ghafla cha mwanafunzi wa shule ya Msingi Manga iliyopo kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani Makete aitwaye Ushindi Fiheke ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia Julai 20 baada ya kuugua mdomo na tumbo kwa muda mfupi

Tumezungumza na Baba Mkubwa wa marehemu muda mchache baada ya maziko ya mtoto huyo yaliyofanyika jana ambaye ameelezea mazingira ya kifo hicho

Afisa mtendaji wa kijiji cha Ujuni Bw. Tumaini Ngogo amesema kumekuwa na minong'ono baada ya kutokea kifo hicho kuwa ni cha kichawi, ambapo amesema wao kama serikali hawana uhakika na taarifa za kuwa kifo hicho sio cha kawaida, lakini akakemea tabia hiyo na kusema kama wapo wanaofanya hivyo waache mara moja tabia hiyo

Sikiliza sauti zao hapa chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo