Matukio ya ukatili wilayani Makete mkoani Njombe yameendelea kutokea ambapo katika kitongoji cha Mang'oto kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani hapa mwili wa mtoto wa kiume aliyetajwa kwa jina moja la John mwenye umri wa miaka miwili umekutwa umetupwa mtoni ukiwa umeharibika vibaya
Kwa mujibu wa mama Mzazi wa marehemu Bi. Vumilia Kyando mkazi wa Bulongwa wilayani hapa ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji hayo amesema tukio hilo limefanyika wiki tatu zilizopita huku yeye akishuhudia na tukio la kuonekana mwili wa marehemu ukiwa majini limetokea Jumamosi Julai kumi na sita mwaka huu majira ya asubuhi
Amesema alimpata mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la Bahati ambaye walianzisha uhusiano wa kimapenzi wakati yeye akifanya kazi ya baa kwenye baa mpya iliyoanzishwa kijijini hapo, ambapo ilionekana kama mtoto huyo anawatinga katika mahusiano yao na ndipo mwanaume huyo alipomshawishi wamuue na yeye akakubali kushiriki mauaji hayo
Bi. Kyando amesema siku ya tukio alipigiwa simu na mumewe huyo waongozane kwenda mtoni kutekeleza mauaji hayo, na kwa maelezo yake amesema walipofika eneo la tukio mpenzi wake alimchukua mtoto na kumfanyia mauaji huku akimwambia mwanamke huyo ambaye ni mama mzazi wa mtoto aangalie watu kama wanapita eneo hilo wasije kuwaona
"Mimi nilikuwa nimemvalisha mwanagu nguo lakini yeye alimvua ndipo akatekeleza mauaji hayo huku mimi nikiwa kwa juu kule naangalia watu kama alivyoniagiza" amesema Vumi

sikiliza sauti hizi hapa chini