Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TAKWIMU
zinaonyesha kwamba mimba za utotoni zimeongezeka kwa wastani wa
asilimia nne kutoka asilimia 23 mwaka 2010,hadi kufikia asilimia
27,mwaka Jana kutokana na kukosa uwekezaji kwa watoto wa kike.
Akizungumza
kwenye mkutano wa Nijali Media Dialogue ulioandaliwa na Shirika la
C-SEMA, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA),Christina Kwayu, amesema
wasichana wenye umri chini ya miaka 18 wamekuwa wakiolewa kwa idadi
kubwa.
Amesema
ndoa hizo zinasababisha kuwepo kwa mimba za utotoni na ndio nas
kufanya wadau wa masuala ya watoto kupigia kelele juu ya sheria ya ndoa
ya mwaka 1971 irekebishwe ili kuweza msichana kutimiza malengo yake.
"Japo
baadhi ya imani ya dini zinasema mtoto chini ya miaka 18 anaweza kuolewa
lakini haijatoa nafasi ya kumlazimisha msichana kuolewa",amesema Kwayu.
Naye Mkurugenzi Wa Shirika la Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti, amesema kati ya watoto watano,watoto wawili wanaolewa hapa nchini.
Amsema
hukumu iliyoyolewa na mahakama kuu kuhusu umri wa mtu kuolewa kuwa ni
miaka 18, itumiwe kama sehemu ya kuwashitaki wale wote wanaooa watoto.
Mtengeti,
mchakato wa kubadilisha sheria ya ndoa umefika katika hatua nzuri na
kuwataka wadau wote kuwa na nguvu ya pamoja katika kumtetea msichana
waTanzania.
Amesema
utekelezaji wa hilo litafanikiwa pale wadau wote wataposhinikiza
wabunge kubadilisha sheria hiyo na kuwataka watunge Sera na sheria
walichukue hilo na kulifanyia kazi.
Kwa
upande wake,Afisa Jinsia kutoka Shirika la Kimataifa la Vijiji vya
Watoto(SOs), Catherine Kasimbazi, alisema kubadilishwa kwa vipengele
ambavyo vina mkandamiza mtoto ni hatua nzuri katika msichana kuweza
kupata utu wake.
Amesema
dhamira ya Nijali ni kuwajali watoto na kwamba sheria ya ndoa
ikibadilishwa usawa kati ya mtoto wa kike na wakiume utakuwepo.
Mkutano
huo ulioandaliwa na Csema kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Australia uliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachama wa Chama
cha Waandishi wa Habari za watoto.
