Mgogoro wa ardhi katika mashamba ya Ludodolelo wilayani Makete mkoani
Njombe umechukua sura mpya baada ya wananchi kutaka kuchoma magari ya
wawekezaji na kuziba barabara huku wakitishia kuvamia mashamba hayo na
kugawana baada ya viongozi wao kuzuiwa kuingia kwenye ukumbi wa kijiji
wakati wawekezaji wakihojiwa na Tume iliyoundwa kuchunguza mgogoro huo.
Hatua hiyo imekuja baada ya diwani na mtendaji wa kata ya Mbalache
wilayani Makete mkoani Njombe kutoruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa
kijiji wakati wawekezaji wa shamba la Ludodolelo kampuni ya Silver lands
na Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe wakihojiwa na tume ya kuchunguza
magogoro huo ambapo wananchi waliweka magogo kuziba barabara na kutaka
kuchoma moto magari ya wawekezaji huku wakitishia kuvamia mashamba hayo.
Kwa upande wao wawekezaji wa shamba la Ludodolelo wamesikitishwa na
vurugu hizo huku Padre Arnord Likiliwike akisema kutaka kuchoma moto
magari si dalili njema na lengo ni kujenga hivyo wanataka amani itawale
katika kutatua mgogoro huo huku meneja wa shamba la Ludodolelo toka
kampuni ya Silver lands Bw. Steven Maina akisema wao wameitwa
kuzungumzia shamba hilo na kwamba nani wanapaswa kushikilia si hoja ya
msingi kwao.
Kaimu Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza mgogoro huo Bw.Joshua Ndyamukama
ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)
wilaya ya Makete amesema kuwa mwekezaji katika
shamba la Ludodolelo kampuni ya Silver lands ilikuja bila kuripoti ofisi
ya kijiji na kata