Makubwa tena: Ndugu wagoma kumzika mwenzao

Ndugu wamesusa kushiriki maziko ya marehemu Andrew
Daffa  kutokana na Mahakama kumpa haki hiyo mjane wake badala ya baba mzazi  aliyetaka yafanyike mkoani Tanga.

Kususa kwa ndugu hao kunatokana na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kutupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na baba wa marehemu huyo akitaka mwili wa mtoto wake kuzikwa kijijini kwao mkoani humo.

Mwili huo umezika  katika makaburi ya Yombo Vituka, Dar es Salaam chini ya ulinzi wa polisi.

Awali, mwili wa Daffa ulizuiwa kuzikwa kutokana na maombi namba 240 ya mwaka 2016 yaliyofunguliwa na baba wa marehemu,  Charles Joseph aliyetaka apewe kibali cha kumzika mwanaye katika Kijiji cha Vigiri mkoani humo kwa madai kuwa alizaliwa huko.

Mvutano huo ulikuja kufuatia mjane wa Daffa, Glory Charles kutaka kupewa haki ya kuzika mwili wa mumewe katika makaburi yaliyopo Yombo Vituka kwa kile alichoieleza eneo hilo ndilo walilozika watoto wao watano.

Kutokana na mvutano huo, Jumanne wiki hii, Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya mwili huo kuzikwa Tanga.

Daffa alifariki dunia Jumatano ya wiki iliyopita katika Hospitali ya Amana.

Hakimu Adolf Sachore amesema chanzo cha familia ni baba, mama na watoto, hivyo mahakama imetoa kibali mwili  huo uzikwe walipozikwa watoto wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo