skip to main |
skip to sidebar
Hali ya wasiwasi imetanda kwenye Vijiji vya Tarafa ya Loliondo

Hali ya wasiwasi imetanda kwenye vijiji vya tarafa ya Loliondo baada ya
watu kumi na sita wakiwemo wenyeviti wawili wa vijiji vya Mondoros na
Keitaro pamoja afisa sheria mfawidhi wa kituo cha sheria na haki za
binadamu mkoa wa Arusha Shilinde Ngalula kudaiwa kukamatwa kwa madai ya
kujihusisha na matendo ya ujasusi huku wananchi wakidai kuwa kinacho
wafanya kukamatwa ni kukataa kutoa ardhi yao kwa wawekzaji kutoka nje ya
nchi.
ITV ilifika kwenye vijiji vya Ketaro Oloipiri Ololosokwani Ololieni
lopol Oldonyowasi Losoito Arusha na kushuhudia ukimya uliyo tawala
kwenye vijiji hivyo huku wananchi wakiogopa kuongea hata na waandishi wa
habari kwa hofu ya kukamatwa.
Kwa upande wake afisa sheria mfawidhi na mkuu wa kituo wa kituo cha
sheria na haki za binadamu mkoa wa Arusha Shilinde Ngalula amesema
alikuja Loliondo kutetea watu waliyo kamatwa na kuelezea alichokutana
nacho.
ITV iliutafuta uongozi wa juu wa mkoa wa Arusha na kubisha hodi kwenye
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda kupata ufafanuzi wa
matukio hayo lakini wasaidizi wake wamesema yupo mkoani Dodoma kwa
shughuli za kiofisi lakini juhudi zaidi za kumpata kiongozi huyo
zinaendelea.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi