Basi la kampuni ya Sikinde Express lililokuwa likotoka Njombe kwenda Makete limepinduka katika kijiji cha Mang'oto kata ya Mang'oto wilayani Makete leo asubuhi
Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili asubuhi ni dereva wa basi la Sikinde kukwepa kugongana uso kwa uso na basi la Mwafrika lililokuwa likitokea Makete kwenda Iringa, baada ya mabasi hayo kukutana kwenye kona huku pia wembamba wa barabara ukichangia kushindwa kupishana
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha licha ya abiria mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja aliyekuwa kwenye basi la Sikinde kuumia sikio lake huku dereva wa basi hilo akiumia mkono wake wa kulia.
Akizungumzia ajali hiyo kwenye eneo la tukio dereva wa basi la Sikinde Bw. Regino Chaula amesema kuwa alikuwa akiendesha basi hilo mwendo wa kawaida lakini alipofika kwenye kalavati lililopo eneo la tukio akakutana na basi la Mwafrika hali iliyomlazimu kukwepa kugongana nalo uso kwa uso hali iliyopelekea kugonga ukingo wa barabara na kisha kupinduka
Kwa upande wake kondakta wa basi hilo Bi Olesta Mwalongo ameelezea namna ajali hiyo ilivyotokea huku akisema wembamba wa barabara umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kupishana vizuri na ajali hiyo kutokea.
Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio leo saa 8 mchana jitihada za kuliondoa basi hilo kwenye eneo la ajali zilikuwa zinaendelea, na kwa mujibu wa mashuhuda basi la Mwafrika liliendelea na safari yake kama kawaida kwa kuwa halikupata madhara

Sikiliza sauti hizi hapa chini