Mtuhumiwa Mohamed Yusuph Ally anayedaiwa kuingiza milioni 7 kwa dakika akipelekwa rumande.
MFANYABIASHARA anayedaiwa kukwepa kodi na kuingiza shilingi milioni 7
kwa dakika amesomewa mashitaka 199 leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar kisha kupelekwa rumande.
Mtuhumiwa huyo aitwaye Mohamed Yusuf Ally alisomewa mashitaka hayo
likiwemo la kugushi na kuwasilisha taarifa za uongo kwa kamishna wa TRA
akidaiwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 15 za Kitanzania.
Watuhumiwa wakitolewa eneo la mahakama.
Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watatu hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Huruma Shaidi aliiahirisha na akasema itatajwa tena Julai 25 mwaka huu
Habari na picha: Denis Mtima

